Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kulifungua rasmi
Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma. Kushoto ni Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad na Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (kulia).
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo, tarehe 15 Oktoba, 2015, amelifungua rasmi jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Rais Kikwete ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa kujenga jengo zuri linaloakisi sifa na heshima ya utendaji wa Ofisi hiyo.
Kwa upande wake CAG, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Nne kwa kuiwezesha ofisi yake na kuongeza uhuru wa ofisi hiyo kwa kuwawezesha kujenga majengo katika mikoa ya Singida, Morogoro na Kilimanjaro.
Ufunguzi huo ulishuhudiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, baadhi ya viongozi waandamizi na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kutoka Makao Makuu na Dodoma. Kwa upande wa Wizara ya Fedha walioshuhudia ni Waziri wa Fedha, Bibi Saada Mkuya na Katibu Mkuu wake, Dkt. Servacius Likwelile.
Jengo hili limekusudiwa kuwa makao makuu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni