Timu ya Arsenal inakabiliwa na
kibarua kigumu cha kufuzu hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya
katika kundi F baada ya kukubali kipigo cha paka mwizi dhidi ya
Bayern Munich.
Washika mtutu hao wa London
walijikuta wakianza kutota kwa maboa 3-0 katika nusu ya kwanza ya
mchezo huo kupitia magoli yaliyofungwa na Robert Lewandowski, Thomas
Muller na David Alaba.
Katika mchezo huo ulioishia kwa
Bayern Munich kuibuka na ushindi wa mbao 5-1, ushindi ambao
unaibakisha Arsenal na pointi sita nyuma ya Bayern na Olympiakos huku
ikiwa na michezo miwili iliyobakia.
Matokeo mengine ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya ni Barcelona 3 - 0 BATE Bor, Chelsea 2 - 1 Dynamo, Roma 3 - 2
Bayer Levkn, Olympiakos 2 - 1 Dinamo, M'bi Tel-Aviv 1 - 3 FC Porto,
KAA Gent 1 - 0 Valencia na Lyon 0 - 2 Zenit St P.
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni