Uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya
Mexico wa kuruhusu kidogo matumizi ya bangi unaweza hatimae kufungua
njia ya kuruhusiwa matumizi ya bangi nchini humo.
Watu wanne kutoka Jamii ya Wamexico
wa Matumizi ya Bangi ya Binafsi kwa Uvumilivu, wataruhusiwa kupanda
bangi yao na kuivuta.
Bangi bado hairuhusiwi kuuzwa Mexico
lakini baadhi ya watu wanasema uamuzi huo wa mahakama utasaidia
kufanikisha kuhalilishwa bangi.
Mexico imekuwa ikigubikwa na
mapigano yanayohusisha magenge ya dawa za kulevya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni