Kiongozi wa Myanmar Bi. Aung San Suu
Kyi amesema atakuwa juu ya rais iwapo chama chake cha National League
for Democracy (NLD) kitashinda uchaguzi wa jumapili.
Chama cha NLD kinatarajiwa kufanya
vizuri katika uchaguzi huo, lakini Bi. Suu Kyi amepigwa marufuku
kushika wadhifa wa urais na Katiba ya nchi hiyo.
Hata hivyo kauli ya Bi. Suu Kyi kuwa
atakuwa juu ya rais inaashiria kuwa analengo la kuhakikisha anaongoza
serikali ya chama chake licha ya kikwazo hicho cha Katiba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni