Na Mwandishi Wetu
BONDIA Ibrahimu Tamba anapanda tena
ulingoni Novemba 22 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Dar es
Salaam kuwania mkanda wa ubingwa na bondia Baraka Mwakansope kutoka
Mbeya Kg 73 mpambano huo wa raundi kumi.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa la
kisasi baada ya mara ya kwanza Tamba kumsambalatisha bondia Maisha
Samsoni wa uko uko Mbeya hivyo Mwakansope amekuja kwa ajili ya
kulipiza kisasi cha kupigwa kwa mwenzake mpambano uliofanyika
mwanzoni mwa mwaka huu.
Mratibu wa mpambano huo Jaffar
Ndame ameongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano
mawili ya ubingwa ambapo bondia Julius Kisalawe atapambana na
Ramadhani Kumbele Kg 51 ubingwa wa Taifa mpambano wa raundi kumi.
Mpambano mwingine utawakutanisha
Bondia Pius Kazaula wa Morogoro atakaepambana na Abdallah Luwanje
wakati bondia chipukizi kutoka Super D Boxing Promotion Vicent
Mbilinyi atakabiliana na Said Tampoo kutoka Bagamoyo.
Aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na
mapambano mengine ya mabondia chipukizi mbali mbali pia kutakuwa na
burudani za kutosha hivyo kawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo wa
masumbwi kuwai ukumbini kwa michezo itanza rasmi kuanzia saa 11 jioni
na kumalizika mnamo saa tano kasoro usiku.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni