Zlatan Ibrahimovic amecheka na nyavu
mara mbili wakati Paris St-Germain ikiongoza kwa pointi 11 kileleni
mwa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, huku ikiipa kipigo
kikali timu ya Toulouse.
Mshambuliaji huyo raia wa Sweden
amefunga mfululizo kwa michezo sita sasa, ambapo alipata goli lake la
kwanza katika mchezo huo baada ya Angel Di Maria kufunga goli kwa
mpira wa adhabu.
Lucas Moura aliifungia Paris
St-Germain goli la tatu kwa kichwa kufuatia krosi ya Gregory van der Wiel, na kisha
kumtengenezea Ibrahmovic bao lake la pili, huku Lavvezi akihitimisha
karamu ya magoli 5-0 katika mchezo huo.
Matokeo mengine ya Ligi Kuu ya
Ufaransa ni Caen 2 - 1 Guingamp, Lille 1 - 1 Bastia, Lorient 4 - 1
Troyes, Montpellier 2 - 1 Nantes na Reims 1 - 2 GFC Ajaccio.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni