Hali ya mtafaruku iliikumba shule ya
msingi ya Balita iliyopo Wilaya ya Mayuge nchini Uganda baada ya
wazazi wenye hasira kuvamia shule hiyo na kuanza kuwachapa bakora
walimu.
Wazazi hao walivamia shule hiyo
Ijumaa jioni baada ya kupata taarifa kuwa mwalimu Robert Gidudu
alimchapa fimbo hadi kufa mwanafunzi Sharifa Nabagala, wa darasa la
sita.
Walimu hao walinusuriwa na polisi
kutoka kituo cha polisi Kati cha Mayuge, ambao walipewa taarifa ya
kichapo hicho waliokuwa wakipatiwa walimu na wazazi wa wanafunzi wa
shule hiyo.
Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo
Moses Mwase, alisema wazazi hao walikuwa na mawe pamoja na fimbo na
walianza kuwapiga walimu kwa kuwatuhuma za kumuua mwanafunzi huyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni