Waziri wa Ardhi wa Kenya
aliyesimamishwa kazi, Bi. Charity Ngilu, amemtuhumu rais Uhuru
Kenyatta kwa mara nyingine kwa kuonyesha upendeleo katika mapambano
dhidi ya rushwa.
Bi. Ngilu amesema kitendo cha rais
kushindwa kumsimamisha kazi Waziri wa Wizara ya Ugatuaji Madaraka Bi.
Anne Waiguru kufuatia tuhuma nzito za rushwa katika wizara yake,
kumeifanya nchi kuwa kituko.
Amesema kuwa heshima ya taifa la
Kenya ipo mashakani na Wakenya wameanza kupoteza imani na serikali
yao katika mapambano dhidi ya rushwa, kutokana na kuwepo upendeleo na
kukosekana utashi wa kisiasa.
Waziri wa Ardhi aliyesimamishwa Bi. Charity Ngilu
Waziri wa Wizara ya Ugatuaji Madaraka Bi. Anne Waiguru



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni