Mgombea urais wa Marekani Donald
Trump amekumbwa na dhahama ya kuzomewa kwa sauti iliyokuwa kimuita
mbaguzi wakati ufunguzi wa shoo ya uchekeshaji jana usiku.
Kitendo hicho kimefanywa na
mchekeshaji Larry David, ambaye alisema ni mzaha katika kupaza sauti
ya kundi la kudai haki za Walatino, waliokerwa na kauli za Bw. Trump
kuhusiana na Wahamiaji wenye asili ya Mexico.
Waandamanaji wenye asili ya Kilatino
walikuwa nje ya studio za NBC Jijini New York wakati shoo hiyo
ikiendelea.
Wakati akitangaza nia ya kuwania
urais kwa tiketi ya chama cha Republican Bw. Trump aliwaelezea
wahamiaji wa Mexico kama wabakaji na wauza dawa za kulevya.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni