Timu ya Chelsea imeanza kwa ushindi
bila ya kocha Jose Mourinho katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya
Uingereza dhidi ya Sunderland ulioishia kwa mabao 3-1 katika dimba la
Stamford Bridge, huku mashabiki wakionekana kuendelea kumtetea
Mourinho.
Mashabiki wa Chelsea walionyesha
wazi kumuunga mkono Mourinho aliyetimuliwa kwa kuwa na mabango ya
kitambaa yanayowalaumu wachezaji kwa kumuangusha kocha huyo, huku
Diego Costa na Cesc Fabregas wakizomewa kabla na baada ya kumalizika
mchezo huo.
Katika mchezo huo Branislav Ivanovic
aliruka juu na kufunga kwa kichwa kikali mnamo dakika ya tani na
kuiongoza Chelsea, mabao mengine ya Chelsea yalifungwa na Pedro
dakika ya 13 na Oscar dakika ya 50 kwa mkwaju wa penati.
Branislav Ivanovic akiwa ameruka juu kupiga kichwa kilichozaa goli
Mpira wa kichwa uliopigwa na mchezaji Branislav Ivanovic ukitinga wavuni
Matokeo mengine:- Everton 2 - 3 Leicester, Man Utd 1 -
2 Norwich, Southampton 0 - 2 Tottenham, Stoke 1 - 2 Crystal Palace na
West Brom 1 - 2 Bournemouth.





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni