.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 20 Desemba 2015

RAPA NICKI MINAJ ATUMBUIZA TAMASHA LILILOPINGWA NA WANAHARAKATI

Rapa wa kike Nicki Minaj amebainisha kuwa yeye ni mbishi, baada ya kutumbuiza kwenye tamasha jana nchini Angola, licha ya wanaharakati wa haki za binadamu kupinga tamasha hilo na kutaka lifutwe.

Rapa huyo ametumbuiza katika Jiji la Luanda katika hafla ya maandalizi ya krismas iliyoandaliwa na kampuni ya Unitel communications, ambayo kwa sehemu inamilikiwa na familia ya kiongozi wa nchi hiyo rais Jose Eduardo dos Santos, ambaye anadaiwa kujilimbikizia mali.

Rais Dos Santos, 73, amekuwa akituhumiwa kwa kuhusika na rushwa, kutumia madaraka vibaya na kutishia wananchi, katika taifa ambalo limemo katika lindi la umasikini, licha ya kuwa la pili kwa uzalishaji mafuta barani Afrika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni