Wanandoa nchini Kenya wamefunga
harusi katika kitanda cha hospitali baada ya ajali kumfanya Bibi
harusi kushindwa kutembea kwa muda, hata hivyo haikuweza kuzuia
kufungwa kwa ndoa yake.
Harusi hiyo iliyofungwa jana ni ya
mfanyabiashara wa Nairobi, James Mwangi (26) na mchumba wake Miariam
Gakenia (31) mtaalam wa mifumo ya komputa, ambapo uongozi wa
hospitali ya Outspan ya Nyeri ilitoa eneo la kufungia ndoa hiyo.
Wapenzi hao wawili ambapo walianza
mahusiano yao kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, walijeruhiwa katika
ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria 14 'matatu' na lori
moja katika barabara kuu ya Nyeri-Nairobi jumanne jioni.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni