Daktari wa mgombea wa
urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Bw. Donald
Trump, amesema mgombea huyo afya yake ipo imara na hana tatizo lolote
la kiafya.
Bw. Trump amekuwa katika shinikizo
la kutoa taarifa ya historia ya hali ya afya yake baada ya wagombea
urais kadhaa wa Marekani kufanya hivyo.
Bw. Trump (69)
ambaye ni tajiri wa majumba, iwapo atapitishwa na chama chake na
kushinda urais wa Marekani atakuwa rais mzee kuwahi kuchaguliwa
katika historia ya Marekani.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni