Mbunge wa Chama Tawala cha Zimbabwe
amefikishwa mahakamani kwa kutoa lugha chafu zikimlenga mke wa rais
Robert Mugabe, Grace wakati alipokuwa akikwaruzana mwanachama
mwenzake wa chama cha ZANU-PF, aliyekuwa amebeba bango lenye picha ya
mke huyo wa rais.
Mbunge huyo Justice Wadyajena,
amefunguliwa shitaka la kutoa lugha chafu kitendo ambacho kilikuwa na
lengo la kuvunja amani, wakati alipofikishwa mbele ya hakimu Lindiwe
Maphosa jana katika mji wa Victoria Falls.
Mwendesha mashtaka Listen Nare
aliiambia mahakama kuwa mbunge huyo alimtolea lugha chafu mwanachama
mwenzake aliyekuwa ameshika bango lenye picha ya Grace Mugabe
lililokuwa limeandikwa maneno ya kuwataka wanachama kumuunga mkono
mke wa rais.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni