Helkopta mbili za kikosi cha Jeshi
la Majini la Marekani zimegongana karibu na kisiwa cha Oahu kilichopo
Hawaii zikiwa kila moja na watu sita.
Ajali hiyo ya kugongana helkopta
hizo imetokea usiku wakati wa mazoezi chanzo cha ajali
hakijajulikana. Mkuu wa walinzi wa Pwani Afisa Sara Moores amesema
mabaki yameonekana baharini.
Kapteni wa Kikosi cha Jeshi la
Majini Timothy Irish amesema zoezi la kuwatafuta wanajeshi na uokoaji
linaendelea pamoja na kubaini zilipo helkopta hizo za mbili aina ya
CH-53.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni