Umoja wa Mataifa umesema kuwa
kunaushahidi kwamba vikosi vya ulinzi vya Burundi vimewabaka wanawake
wakati vikifanya msako kwenye nyumba za wanaume wanashukiwa kuwa ni
viongozi wa upinzani.
Umoja wa Mataifa umesema
umeandikisha maelezo ya matukio 13 ya ubakaji ambapo vikosi vya
ulinzi vya Burundi viliwatenganisha wanawake na kuwabaka.
Vikosi hivyo vya ulinzi pia
vimedaiwa kuteka, kutesa na kuwauwa makumi ya wanaume taarifa ya
umoja huo imesema.
Wakati huo huo mahakama imewahukumu
majenerali wanne kifungo cha maisha jela kwa kujaribu kumpindua rais
Pierre Nkurunziza mwezi Mei mwaka jana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni