Jeshi la Ulinzi Kenya (KDF)
limepeleka helkopta na ndege za kivita kuwashambulia wapiganaji wa
kundi la Al-Shabaab baada ya kundi hilo la kigaidi kuishambulia kambi
ya jeshi ya El-Adde huko Gado nchini Somalia na kuuwa idadi ya
wanajeshi ambayo haijajulikana kwa sasa.
Rais Uhuru Kenyatta, ambaye pia ni
Amiri Jeshi Mkuu amewapongeza wanajeshi wa Kenya wa Kenya waliouwawa
kwa kusema wamekufa kishujaa kutokana na kufa wakiilinda Kenya dhidi
ya maadui.
Rais Kenyatta amesema vikosi vya
wanajeshi wa Kenya vitaendelea kuwapo Somalia kuendelea kupambana na
wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab hadi hapo kundi hilo la kigaidi
litakapo dhibitiwa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni