Nchi ya Iran inafikiria kununua
ndege kutoka kwa kampuni ya kutengeneza ndege ya Marekani ya Boeing
wakati huu ikijipanga kuimarisha sekta ya usafiri wa anga, baada ya
kuondolewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.
Naibu Waziri wa Usafiri wa Iran Bw.
Asghar Fakhrieh Kashan ameliambia shirika la habari la Reuters
kwamba Iran inatarajia kununua ndege 100.
Vikwazo vya Umoja wa Mataifa
viliondolewa wiki moja iliyopita, na kutoa fursa shirika la ndege la
Airbus kufanya mazungumzo ya kuiuzia Iran ndege 114.
Vikwazo vya kibiashara vya Marekani
kwa Iran bado vipo, lakini kampuni ya Boeing inaweza kuomba
kuondolewa ili nayo ifanye biashara ya kuuizia ndege Iran.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni