.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 25 Januari 2016

UINGEREZA YAFIKIRIA KUWACHUKUA WATOTO WAKIMBIZI

Serikali ya Uingereza inafikiria juu ya wito wa kutakiwa kuwachukua watoto wakimbizi wasio na walezi wala waangalizi ambao wameingia barani Ulaya, Waziri mmoja wa nchi hiyo amesema.

Taasisi za misaada zimekuwa zikiitaka Uingereza kuwachukua watoto hao wakimbizi 3,000 ikiwa kama sehemu ya muitikio wa msaada kwa mgogoro wa Syria.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Justine Greening amesema mawaziri wanafikiria iwapo wanaweza kufanya jambo la ziada kwa watoto hao wakimbizi wasio na waangalizi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni