Mamia ya nakala za bajeti ya Nigeria
ya mwaka 2016 zimepotea bungeni katika bunge la nchi hiyo, kwa mujibu
wa mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Baraza la Seneti la Nigeria
limeshindwa kuanza kujadili pendekezo la bajeti hiyo kutokana na
kupotea kwa nakala za bajei hiyo.
Kuchelewa kujadiliwa kwa bajeti hiyo
kutachangia hali ya uchumi wa Nigeria kuwa mbaya zaidi, kutokana na
taifa hilo kukumbwa na athari za kushuka kwa bei ya mafuta duniani.
Rais Muhammadu Buhari aliwasilisha
nakala za bajeti yake hiyo ya kwanza tangu aingie madarakani kwa
mabunge yote mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni