Goli la dakika ya 90 la Paul Dummett
liliifanya Newcastle kuinyima ushindi Manchester United ili kuweza
kuwa na pointi sawa na Tottenham katika nafasi ya nne ya msimamo wa
Ligi Kuu ya Uingereza.
Katika mchezo huo ulioishia kwa sare
ya mabao 3-3, Wayne Rooney aliifungia Manchester united bao la kwanza
kwa njia ya penati na kisha Jesse Lingard kuongeza la pili kabla ya
Georginio Wijnaldum na Aleksandar kusawazisha.
Wachezaji wa Manchester United wakishangilia bao lililofungwa na Wayne Rooney
Jesse Lingard akipachika bao la pili la Manchester United
Katika mchezo mwingine timu
iliyomkiani mwa msimamo wa ligi ya Aston Villa ilipata ushindi wake
wa kwanza ikiwa chini ya Remi Garde baada ya kosa la kizembe
lililofanywa na kipa wa Crystal Palace, Wayne Hennessey.
Hennessey aliruhusu kizembe mpira wa
kona uliopigwa kichwa na Joleon Lescott kumpita na kuandika bao pekee
katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Uingereza. Matokeo mengine ya jana
ni Bournemouth 1 - 3 West Ham.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni