Mke wa mwanaharakati maarufu wa haki
za binadamu nchini Saudi Arabia, Waleed Abu al-Khair amekamatwa,
wanaharakati wa nchi hiyo wamesema.
Mke huyo wa al-Khair, Bi. Samar
Badawi alikamatwa kwa madai ya kumiliki akaunti ya twitta inayotoa
wito wa kutaka kuachiwa huru kwa mumewe.
Shirika la Amnesty International
limekiita kitendo cha kukamatwa Bi. Badawi kama mfanu wa hivi
karibuni wa namna Saudi Arabia inavyojaribu kuzima haki za binadamu.
Abu al-Khair amehukumiwa kifungo cha
miaka 15 jela kwa kudharau mamlaka ya Saudi Arabia tangu mwaka 2014.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni