Miili ya kwanza ya wanajeshi wa
Kenya waliouwawa nchini Somalia imewasili na kupokelewa na Waziri wa
Ulinzi wa Kenya Bi. Raychelle Omamo, ambaye amesema zoezi la
kuwatafuta wanajeshi wengine linaendelea.
Miili hiyo iliyowekwa kwenye
majeneza manne yaliyofunikwa kwa bendera ya taifa la Kenya,
imepokelewa na Bi. Omamo pamoja na maafisa waandamizi wa jeshi
akiwemo Mkuu wa Majeshi Bw. Samson Mwathethe jana saa nne usiku
katika uwanja wa ndege wa Wilson Jijini Nairobi.
Viongozi wa dini ya kikristo wawili
na Imamu mmoja walisoma dua ya kuwaombea wanajeshi hao waliokufa
katika shambulio lililofanywa kwenye kambi ya jeshi na kundi la
Al-Shabaab nchini Somalia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni