Muwania urais wa Marekani Bw. Donald
Trump amekejeliwa na wagombea wenzake wa chama cha Republican katika
mdahalo uliorushwa kwenye Televisheni kutokana na mgogoro wake na
kituo cha Fox News.
Mgombea huyo machachari aliamua
kujitoa kwenye mdahalo huo kutokana kituo hicho kukataa kumuondoa
mtangazaji Megyn Kelly kuongoza mdahalo, ambaye Bw. Trump anamtuhumu
kwa kuwa na upendeleo.
Badala yake bilionea Bw. Trump
aliitisha mkutano wa hadhara karibu na mdahalo huo kwa ajili ya
kuwaenzi mavetenari wa vita, jambo ambalo lilitishia kuathria idadi
ya watu iliyofuatilia mdahalo huo.
Jumatatu ya wiki ijayo huko Iowa,
wapigakura wanatapiga kura kuwateuwa mgombea wao wa urais wa vyama
vyao.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni