.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Januari 2016

WAHAMIAJI 39 WAFA MAJI WAKIKATIZA BAHARINI KWENDA UGIRIKI

Wahamiaji wapatao 39 wakiwemo watoto wamekufa maji wakijaribu kukatiza bahari ya Aegean kutokea Uturuki kwenda Ugiriki, vikosi vya ulinzi vya pwani vimesema.

Zaidi ya watu 60 wameokolewa kutoka baharini karibu na eneo la Ayvacik nchini Uturuki. Wenyeji wa eneo hilo wamesema wanatarajia kuongezeka kwa idadi ya vifo baada ya kukaguliwa bodi lao lililozama.

Maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wamekuwa wakiendelea kutumia safari hatari ya kukatiza baharini kutoka Uturuki kwenda Ugiriki ili kuingia mataifa ya Ulaya kaskazini.

Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) limesema Ijumaa wahamiaji 244 wamekufa maji katika bahari ya Mediterranean katika mwaka huu hada sasa huku 55,568 wakiwasili wanapoenda.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni