Muwania urais wa Marekani Bi. Hillary Clinton amepata ushindi
mkubwa dhidi ya Bernie Sanders huko Carolina Kusini katika kura za
maoni kwa upande wa wagombea urais wa chama cha Democratic.
Ushindi wa Bi. Clinton ulikuwa ukitarajiwa mno na pia unampa
kasi katika kuelekea siku ya Jumanne ambayo kura za maoni zitafanyika
kwenye majimbo 11.
Akiongea na wafuasi wake huku akishangiliwa Bi. Clinton amesema
kesho kampeni za kuwania urais zitafanyika kitaifa. Sander
amempongeza Clinton na kusema kuwa kampeni ndio kwanza zinaanza.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni