.
.
.
.
.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga
|
TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.
mbani
NYUMBANI
HABARI
SIASA
MICHEZO
BURUDANI
TABASAMU
KIMATAIFA
Alhamisi, 18 Februari 2016
KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AKIPONGEZA KIWANDA CHA VIATU GEREZA KARANGA MJINI MOSHI KWA UTENGENEZAJI WA VIATU BORA NCHINI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia aliyevaa kiraia) akiingia ndani ya Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi. Rwegasira amefanya ziara kwa kukitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo wakati Kiongozi huyo wa Wizara alipowasili katika ofisi za Magereza Mkoa, mjini Moshi.
Fundi wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi, Hashim Rashid akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) jinsi buti la Jeshi linavyotengenezwa ndani ya kiwanda hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia buti la Jeshi lililotengenezwa na Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi. Kiwanda hicho kinatengenezwa viatu vya aina mbalimbali. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Venance Kayombo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na Maafisa wa Magereza, Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji mara baada ya kumaliza kukitembelea Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi. Rwegasira alikipongeza kiwanda hicho na kulitaka Jeshi la Magereza kuongeza juhudi zaidi katika uzalishaji wa viatu.
Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga Moshi, mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Anderson James akimpa zawadi ya viatu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya kufanya ziara ya kukikagua kiwanda hicho pamoja na kujifunza jinsi ya utengenezaji wa viatu unavyofanyika. Kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni ( Atom )
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni