.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 14 Februari 2016

KOCHA WA VALENCIA GARY NEVILLE HATIMAE APATA USHINDI WA KWANZA LA LIGA

Kocha wa Valencia, Gary Neville hatimae amepata ushindi wake wa kwanza tangu aanze kuinoa timu hiyo ya Hispania baada ya kuifunga Espanyol mabao 2-1 jana usiku katika mchezo wa La Liga.

Katika mchezo huo beki raia wa Costa Rica, Oscar Duarte aliruka juu na kufunga goli la kichwa na kuwafanya wageni kuongoza kwa goli moja mnamo dakika ya 52 ya mchezo huo.

Hata hivyo Alvaro Negredo alisawazisha katika dakika ya 71, kabla ya Mrusi Denis Cheryshev kufungwa kwa mpira wa kichwa zikiwa zimebakia dakika tano na kuipa ushindi Valencia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni