Goli la Leonardo Ulloa katika dakika
ya 89 limeongeza uongozi wa Leicester City wa Ligi Kuu ya Uingereza
na kufikisha tofauti ya pointi tano, na kuinyima Norwich sare ambayo
walikuwa wakistahili kupata.
Timu ya Norwich mapema ilikuwa na
nafasi nzuri ya kufunga lakini Cameron Jerome alikosa kwa kupiga
kichwa kilichotoka nje huku shuti lililopigwa na Nathan Redmond
likitoka nje.
Jerome akipiga kichwa kilichopanguliwa na kipa Schmeichel
Nayo timu ya Chelsea imekwea hadi
katika nafasi ya 11 ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya
kutokea nyuma kwa kufungwa bao moja na Southampton na kuibuka na
ushindi wa mabao 2-1.
Katika mchezo huo goli la
Southampton lilifungwa aliyeruka juu na kutumbukiza mpira wa kichwa
wavuni, kabla ya Cesc Fabregas kusawazisha na baadae Branislav
Ivanovic kufunga kwa kichwa bao la pili.
Cesc Fabregas akipiga shuti la kupinda lililotinga wavuni




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni