.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 26 Februari 2016

MCHEZO WA FA BAINA YA ARSENAL NA HULL CITY KUKIUKA SHERIA YA UEFA

Chama cha Soka cha Uingereza kimesema ratiba ya michezo iliyofuatana kwa karibu haiwezi kubadilishwa, hali inayokinzania na miongozo ya UEFA ili kuipa fursa Arsenal na Hull kumaliza mchezo wa FA kwanza kabla ya usiku wa Ligi ya Mabigwa Ulaya.

Mchezo wa marudio wa FA mzunguko wa tano utakaoonyeshwa Live BT Sport, siku ya jumanne utagongana na mechi ya Real Madrid na Roma pamoja na Wolfsburg na Gent za michuano ya Mabingwa Ulaya.

Mchezo huo wa Arsenal na Hull utakaopigwa kwenye dimba la KC stadium utaanza majira ya saa moja usiku majira ya Uingereza, lakini hata hivyo kwa kufanya hivyo inavunjwa sheria ya UEFA inayotaka michezo ya ndani kuisha dakika 30 kabla ya kuanza mchezo wa Mabingwa wa Ulaya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni