Lionel Messi na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Argentina
wameonekana kuwa wenye furaha mno katika mazoezi ya kujiandaa na
mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia 2018 dhidi ya
Chile utakaofanyika Santiago.
Nyota huyo anayechezea timu ya Barcelona ya Hispania hakucheza
na timu ya taifa tangu Julai 2015, huku akiikosa michezo yote ya
kampeni ya kuwania kufuzu michuano, na kuifanya timu hiyo kuwa na
wakati mgumu bila yeye.
Wachezaji wa Argentina wakiwa na furaha wakati wakifanya mazoezi yao
Mazoezi yao yaliambatana na adhabu za mizaha za kuchapana makofi kichwani kama inavyoonekana hapa



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni