Kinda Marcus Rashford ameipatia ushindi muhimu Manchester
United dhidi ya wapinzani wao wa jadi katika Jiji la Manchester timu
ya Manchester City.
Mchezaji huyo mwenye miaka 18 alipokea pasi ya Juan Mata na
kumalizia kwa utulivu shuti la kuzungusha baada ya kumpita beki Martin
Demichelis katika dakika ya 15 na kuandika bao pekee.
Sergio Aguero alikosa goli la kusawazisha baada ya kichwa chake
alichopiga kugonga mwamba akiunganisha krosi ya Yaya Toure.
Marcus Rashford akipiga mpira uliojaa wavuni na kumpita kipa Joe Hart
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni