.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 25 Machi 2016

MSHAMBULIAJI VETERANI WA ATHLETIC BILBAO AIOKOA HISPANIA ISIZAME

Mshambuliaji veterani wa Athletic Bilbao, Aritz Aduriz, ameanza kwa kishindo mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa kupachika bao na kuwapatia sare muhimu mabingwa watetezi wa Bara la Ulaya timu ya Hispania.

Katika mchezo huo Italia ilikuwa ya kwanza kupachika bao kupitia kwa winga wa timu ya Napoli Lorenzo Insigne aliyepachika bao safi kufuatia mashambulizi ya kushitukiza.

Lakini Aduriz mwenye miaka 35, na ambaye amefunga mabao 31 katika ligi ya La Liga akiwa na Athletic Bilbao, alisawazisha bao hilo dakika mbili baadae na matokeo kuwa sare ya bao 1-1.
                                 Aritz Aduriz akiteleza na kupachika bao la kusawazisha
              Lorenzo Insigne akimpoteza kipa David De Gea na kupachika bao la kwanza

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni