.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 20 Machi 2016

MTUHUMIWA WA MASHAMBULIZI YA PARIS ASEMA ALITAKA KUJILIPUA AFE

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya Paris Salah Abdeslam amekiri kuwa alikuwa anataka kujilipua ajiuwe, lakini baadaye alibadili mawazo, waendesha mashtaka wa Ufaransa wamesema.

Abdeslam amefunguliwa mashtaka ya ugaidi nchini Ubelgiji, siku moja tu baada ya kukamatwa katika msako.

Wakili wake amesema mtuhumiwa huyo atapinga kupelekwa Ufaransa kushtakiwa kwa kuhusika na mashambulizi ya Paris, lakini ameonyesha ushirikiano kwa polisi.

Mashambulizi ya Paris yaliyofanyika Novemba mwaka jana yalisababisha vifo vya watu 130 na makumi kujeruhiwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni