Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda(kulia) na Meneja Mkuu wa
Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (wa pili kulia),wakiwa wameketi kwenye
moja ya madawati 500 yalikabidhiwa na kampuni ya Tigo kwa shule za
msingi 10 jijini Dar es Salaam jana. Wengine katika picha ni Mkurugenzi
wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles (wa tatu kulia)na Kaimu
Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Dkt. Aziz Msuya(kushoto).
|
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
|
Mwanafunzi Saidat Proches akishukuru mara baada ya makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
|
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akiongea na walimu na wananchi mara baada makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
|
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiteta jambo na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
|
Wanafunzi wa shule ya msingi kawawa wakishuhudia makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Machi 22 2016 Dar es Salaam: Kampuni
ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya
shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es
Salaam ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali
kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.
Akizungumza
leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi
Kawawa iliyopo katika kata ya Mabibo katika manispaa ya Kinondoni,
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema mchango huo ni sehemu ya
utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada
mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.
“Mchango
huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika
kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini
kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga
viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo
madaktari, wahandisi na wengineo, "amesema Gutierrez.
Gutierrez
amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika
shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na
kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu
mbalimbali nchini siku za zijazo.
Makabidhiano
yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye
alisema madawati hayo 500 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto
katika Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga
mkono zoezi hilo.
“Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu
kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la
ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa
Dar es Salaam. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 500
yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo
kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Makonda.
|
|
|
|
|
|
|
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni