Polisi nchini Hispania wamemkamata
raia wa Morocco katika kisiwa cha Majorca hii leo kwa kushukiwa kuwa
na uhusiano na wapiganaji wa kundi la Dola ya Kiislam (IS).
Picha zilizopatikana zinamuonyesha
mtu huyo mwanaume ambaye hakutajwa jina lake, akichukuliwa na maafisa
usalama na kuingizwa kwenye gari huku sura yake ikiwa imefunikwa.
Mtuhumiwa huyo anatuhimiwa kwa
kuandikisha wapiganaji kujiunga na IS nchini Syria na Irak, pamoja na
kusimamia uwezekano wa kufanya mashambulizi Hispania na nchi za
Ulaya.
Polisi wakimuingiza ndani ya gari mtuhumiwa wa ugaidi ndani ya gari
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni