.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 15 Aprili 2016

TIMU YA SEVILLA YATINGA NUSU FAINALI YA UROPA KWA USHINDI WA MATUTA

Timu ya Sevilla inaendelea kupambana kutinga fainali za Uropa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya jana kuibuka na ushindi wa penati 5-4 dhidi ya Athletic Bilbao na kutinga nusu fainali ya ligi ya Uropa.

Ilikuwa mchezaji Kevin Gameiro ndiye aliyefunga penati iliyoamua matokeo ya mchezo huo baada ya penati nne za kila upande kutinga wavuni huku kiungo wa Athletic Bilbao Benat akikosa penati.

Kwa ushindi huo ambao ulitokana na matokeo ya dakika tisini ya michezo yote miwili kuwa mabao 3-3, Sevilla sasa inaungana na Liverpool, Villarreal pamoja na Shakhtar Donetsk katika nusu fainali ya Ligi ya Uropa. 
   Iker Muniain akifuatilia mpira uliopigwa na Aduriz uliomzidi kipa na kujaa wavuni
 Joto la mchezo lilipanda wakati wa kupiga matuta kiasi cha wachezaji kushikana mashati

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni