Kocha wa Bayern Munich, Pep
Guardiola, alijikuta kitota kwa kumwagiwa bia wakati akisherehekea na
wachezaji wake ubingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani kwa ushindi wa magoli
3-1 dhidi ya Hannover.
Kocha huyo ambaye anajiunga na
Manchester City msimu ujao, timu yake ilishakuwa imelitwaa taji hilo
hata kabla ya mchezo huo wa jana, ambao Robert Lewandowski alikuwa wa
kwanza kuifungia Bayern goli la kwanza na kuweka rekodi ya kufunga
magoli 30 katika msimu huu.
Kiungo wa Ujerumani, Mario Gotze,
aliongeza la pili kwa jitihada binafsi nzuri, na kisha kuongeza la
tatu katika kipindi cha pili kabla ya Artur Sobiech hajaifungia
Hannover goli pekee katika mchezo huo.
Cheers ya ubingwa kocha Pep Guardiola akigongesha glasi na mchezaji wake
Wachezaji wa Bayern Munich wakimwagia bia kocha wao Pep Guardiola
Kocha Pep Guardiola akimwagia bia mmoja wa watumishi wa Beyern Munich




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni