Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic
amepachika magoli mawili katika mchezo wake wa mwisho akiwa na Paris
St-Germain walioibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Nantes na
kukabidhiwa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufanrasa.
Nyota huyo wa Paris St-Germain
anayeongoza kwa kuifungia magoli mengi timu hiyo anayeondoka kwenye
timu hiyo katika majira ya msimu wa joto, alilazimisha mchezo
kusimama baada ya dakika kumi wakati mashabiki wa PSG waliposimama na
kumpongeza kwa mafanikio.
Kwa kufunga magoli mawili katika
mchezo wa jana Ibrahimovic amevunja rekodi nyingine ya klabu hiyo,
kwa kuwa mchezaji aliyeifungia PSG magoli mengi katika ligi kwa msimu
mmoja ambapo amefunga magoli 38.
Zlatan Ibrahimovic akiwa amenyanyua juu kombe la Ligi Kuu ya Ufaransa baada ya kutawazwa mabingwa
Zlatan Ibrahimovic akiwa amewabeba watoto wawili waliovaa jezi zenye ujumbe maalum kwake



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni