Serena Williams amemshinda Mmarekani
mwenzake, Madison Keys, kwa seti zote na kutwaa ubingwa wa michuano
ya wazi ya Italia, ikiwa ni taji lake la kwanza tangu miezi tisa
kupita bila kikombe.
Mchezaji huyo namba moja duniani
katika viwango vya tenesi kwa wanawake, alimshinda Mmarekani mwenzake
huyo kwa seti 7-6 (7-5) 6-3 na kutwaa ubingwa wa michuano ya Roma kwa
mara ya nne tangu mwaka 2002.
Williams, 34, kwa mara ya mwisho
alishinda taji kwenye michuano ya Cincinnati mwezi Agosti, tangu
wakati huo amepoteza michezo ya fainali ya Marekani, Australian
pamoja na ya Indian Wells.
Mambo ya Selfie: Serena Williams akijipiga selfie na kombe lake
Oops! kombe likimtereza Serena Williams na mfuniko wake kuanguka



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni