Timu ya taifa la Albania imepata
ushindi wake wa kwanza katika michuano ya kimataifa huko Lyon dhidi
ya Romania na kupata matumaini ya uwezekano wa kutinga hatua ya 16
bora ya michuano ya Euro 2016.
Timu hiyo inayonolewa na Giovanni de
Biasi imemaliza katika nafasi ya tatu kundi A, na sasa watabidi
kungojea iwapo wataibuka namba tatu bora kati ya timu nne
zinazoshiriki michuano hiyo.
Katika mchezo huo mchezaji wa FC
Zurich, Armando Sadiku, aliifungia Abania goli pekee katika mchezo
huo, baada ya kupiga mpira wa kichwa uliomshinda golikipa wa Romania
Ciprian Tatarusanu na kujaa wavuni.
Armando Sadiku akiifungia Albania goli pekee katika mchezo huo
Ermir Lenjani akikosa goli la wazi baada ya kupaisha mpira juu



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni