Watu sita wameuwawa kaskazini mwa
Mexico katika mapambano baina walimu waliokuwa wakiandamana na
polisi.
Katika mapambano hayo watu wengine
50, wakiwemo maafisa polisi wamejeruhiwa.
Tukio hilo limetokea katika jimbo la
Oaxaca, ambako viongozi wa juu wawili wa chama cha walimu walikamatwa
wiki iliyopita kwa tuhuma za rushwa.
Wanachama wa chama hicho cha walimu
cha CNTE, ambacho kinahistoria ya uanaharakati makali, wamefunga
barabara kusini mwa Mexico tangu viongozi wao wakamatwe.
Athari za ghasi za maandamano hayo ya walimu katika jimbo la Oaxaca
Basi likiwa linateketea kwa moto kufuatia ghasi za maandamano hayo ya walimu kupinga viongozi wao kukamatwa



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni