Bi. Hillary Clinton ameelekea
kushinda kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa urais
wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic baada ya kufikisha
idadi ya wajumbe wanaohitaji.
Kwa mujibu wa shirika la habari la
AP idadi ya wajumbe aliopata Bi. Clinton imefikia 2,383, idadi ambayo
inatosha kabisa kumfanya kuteuliwa kuwania urais wa Marekani na chama
cha Democratic.
Iwapo atapitishwa kuwania urais
katika mkutano mkuu wa chama cha Democratic Julai, Bi. Clinton
mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwania urais Marekani na moja ya chama
kikuu nchini humo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni