Mtoto wa kiume nchini Japan ambaye
alipotea kwa siku sita kwenye msitu baada ya wazazi wake kumtelekeza
kama sehemu ya adhabu, ametoka hospitali, na kusema amewasamehe
wazazi wake.
Baba wa mtoto huyo Takayuki Tanooka,
44, na mkewe walimuacha mtoto Yamato Tanooka kando ya barabara
kwenye kisiwa cha kaskazini cha Hokkaido Mei 28 kama adhabu kutokana
na kuwa mtukutu.
Wazazi hao waliporejea katika eneo
walilomuacha hawakumkuta, na kuibua msako mkali ambao ulifanikisha
kumpata mtoto huyo akiwa kwenye kambi ya jeshi, iliyo jirani na msitu
huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni