Tamasha la mwaka la kula mbwa
limeanza kusini mwa China, huku kukiwepo kwa pingamizi ndani ya nchi
na kimataifa kupinga kufanyika tamasha hilo.
Wakati wa tamasha hilo jumla ya mbwa
10,000 na paka huuwawa na kuliwa nyama zao, wakati wote wa tamasha
hilo la siku 10 huko Yulin, China
Wanaharakati wa haki za wanyama
wanasema tamasha hilo linafanya ukatili kwa wanyama hao na tayari
saini milioni 11 zimekusanywa kulipinga.
Maafisa wa Serikali za Mitaa za
Yulin wamesema hawaungi mkono sherehe hizo, ila zinazoandaliwa na
wafanyabishara binafsi.
Nyama ya Mbwa ikiandaliwa tayari kwa kuliwa wakati wa tamasha hilo


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni