Waumini
na mashabiki wa Muhammed Ali wanahudhuria kisomo maalum na kumuenzi
bondia huyo maarufu mkongwe katika mji wa nyumbani kwao Louisville,
Kentucky.
Familia
yake imesema kisomo hicho cha siku mbili hadi kesho yatakapofanyika
maziko, ilikuwa ni mbango wa marehemu Ali aliyouanda mwaka mmoja
kabla ya kifo chake.
Ali
aliomba kufanyiwa kisomo hicho kwa imani ya Kiislam, kiitwacho
Jenazah, kama sehemu ya mafundisho kwa waumini kwa mujibu wa Imamu
Zaid Shakir anayeongoza kisomo hicho.
Tiketi 15 za kuhudhuria kisomo hicho na maziko ya Muhammed Ali zimetolewa bure kwa watu, lakini kuna tiketi zinadaiwa kuingizwa sokoni na kuuzwa na wajanja.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni