Muwania
urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican Donald Trump, amemchagua
Gavana wa Indiana Mike Pence kuwa mgombea mwenza wake.
Kambi
ya kampeni ya Trump ilipanga kutangaza chagua lake hii leo, lakini
imehairisha kutokana na shambulizi la Nice Ufaransa.
Vyanzo
vilivyo karibu na kambi ya kampeni ya Trump, vimekiambia chombo cha
habari cha ABC News kwamba Bw. Pence amekubali uteuzi huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni