Mwanaume
kutoka jamii ya Dalit nchini India ameuwawa kwa kukatwa kichwa yeye
na mkewe katika jimbo la Uttar Pradesh kufuatia kushindwa kulipa deni
la biskuti zenye thamani ya fedha ya India rupee 15.
Polisi
nchini India wamesema wanandoa hao wameuwawa na mfanyabiashara wa
duka hilo hapo jana baada ya kumuambia mmiliki wake wanahitaji muda
zaidi kuweza kulilipa deni hilo.
Polisi
wameeleza zaidi wanandoa hao walisimamishwa na mmiliki wa duka Ashock
Mishra aliyewashinikiza kulilipa deni hilo la pakiti tatu za biskuti
walizowanunulia watoto wao watatu siku chache zilizopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni