Mtu
mwenye bomu amejilipua jana usiku karibu na tamasha la muziki nchini
Ujerumani, likiwa ni tukio la tatu la mashambulizi yaliyomwaga damu
katika wiki iliyomalizika.
Mwanaume
raia wa Syria, mwenye umri wa miaka 27 aliyenyima hifadhi nchini
Ujerumani, amewajeruhi watu 12, kwenye baa iliyojaa watu huko Anbach,
karibu na Nuremberg.
Mhamiaji
huyo ambaye jina lake halijafahamika mara moja alizuiwa kuingia
kwenye tamasha la wazi lililokuwa na watu 2,500, kutokana na kutokuwa
na tiketi.
Hata
hivyo alienda katika eneo la baa iliyopo katika eneo hilo na kisha
kulipua bomu lililotengenezwa kienyeji kwa vyuma na misumari, na
kujeruhi watu 12 ambapo yeye alikufa.
Polisi akichunguza begi la mgongoni linaloshukiwa kuwa lilikuwa na bomu
Watu wakiwa wametaharuki baada ya kutokea tukio hilo la mlipuko wa bomu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni