Mikosi
imezidi kumuandama mwanamuziki nyota barani Afrika Koffi Olomide
baada ya tamasha lake la Zambia kufutwa kufuatia tukio la kumpiga
dansa wake mwanamke Jijini Nairobi siku ya Ijumaa.
Msanii
huyo Mkongo alipangiwa kufanya onesho katika maadhimisho ya 90 ya
Jumuiya ya Kilimo na Biashara nchini Zambia.
Rais
wa Kamati ya Maadhimisho hayo Ben Shoko amesema jana kufutwa kwa shoo
Olomide kunafuatia kitendo chake cha kumpiga dansa wake kwenye uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Koffi
Olomide aliondolewa kwa nguvu Kenya na kurejeshwa Jijiji Kinshasa,
DRC baada ya kukamatwa Ijumaa na kulala ruamande katika kituo cha
polisi cha uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni